Ndugu Msomaji Karibu katika tovuti rasmi ya Mkoa wa Singida. Mkoa wa Singida upo katikati ya Tanzania Bara. Mji wake Mkuu ni Singida na ni njia panda muhimu kwa usafiri wa barabara kwenda Kaskazini, Magharibi, Kusini na Mashariki.
Singida inapakana na Mkoa wa Manyara kwa upande wa Kaskazini, Mkoa wa Dodoma upande wa Mashariki, Mikoa ya Mbeya na Iringa upande wa Kusini na Mikoa ya Tabora na Simiyu upande wa Magharibi.
Mkoa wa Singida ulianzishwa rasmi tarehe 15 Oktoba, 1963 ambapo kabla ya hapo ulikuwa ni Wilaya ya Jimbo la Kati (Central Province) uliojumuisha Mkoa wa Dodoma.
Mkoa wa Singida uko katikati ya Tanzania, kati ya Longitudo 33027’5’’ na 35026’0’’ mashariki ya Greenwich, na kati ya latitudo 3052’ na 7034’ Kusini mwa Ikweta.
Mkoani Singida ndipo kuna eneo eneo rasmi ambalo lilibainishwa na vipimo vya kitaalamu vyenye namba 9305404.35, 698978.015 kuwa ni katikati mwa Tanzania bara yaani Central point of Tanganyika, ambapo ni katika kitongoji cha Darajani, Kijiji cha Chisingisa kilichopo kata ya Sasilo, tarafa ya Nkonk’o Wilaya ya Manyoni.
Mkoa wa Singida una Wilaya 5 ambazo ni Singida, Iramba, Manyoni, Mkalama na Ikungi; zenye Halmashauri 7 za Singida, Singida Manispaa, Iramba, Manyoni, Mkalama, Ikungi na Itigi. Aidha Mkoa una Tarafa 21, kata 136, Vijiji 442, vitongoji 2,309 na majimbo ya uchaguzi 8.
Ukubwa wa eneo la Mkoa wa Singida ni kilomita za mraba 49,341 sawa na asilimia 6 ya eneo la Tanzania Bara ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 11,340 zinafaa kwa kilimo sawa na asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa.
Kwa upande wa hali ya hewa Mkoa wa Singida hupata mvua kwa kipindi kimoja cha mwaka (mwezi Novemba hadi Aprili) kwa wastani wa milimita 500 – 800 kwa mwaka na wastani wa hali ya hewa ni nyuzi joto 15 – 30 kutegemea msimu na mwinuko wa ardhi. Kutokana na hali ya hewa, Mkoa wa Singida ni miongoni mwa Mikoa iliyopo kwenye ukanda wa unaopata mvua kidogo.
Kwa miaka ya karibuni wastani wa mvua umekuwa ukipungua kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kote Duniani. Kwa mfano mwaka 2008/2009 kiasi cha mvua kilichorekodiwa katika kituo cha hali ya hewa Singida ni mm 778, mwaka 2009/2010 mm 641 na mwaka 2010/2011 mm 425.7, mwaka 2011/2012 mm 582 na mwaka 2012/2013 mm 821.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Singida ni 1,370,637 ikiwa wanaume ni 677,995 na wanawake ni 692,642 huku kaya zikikadiriwa kuwa 225,670 ambapo kaya 189,115 zinajishughulisha na kilimo.
Shughuli za kiuchumi Mkoani Singida ni pamoja na kilimo ambacho huajiri wastani wa asilimia 86 ya wakazi wote. Mazao ya kipaumbele kwa upande wa chakula ni uwele, mtama, mihogo na viazi vitamu na kwa upande wa mazao ya biashara ni alizeti, vitunguu, pamba na ufuta. Shughuli nyingine za uzalishaji mali ni ufugaji, uchimbaji mdogo wa madini, viwanda vidogo na biashara.
Pato la Mkoa ni Sh. 978,701,000 huku pato la mwananchi likiwa ni Sh. 697, 667 kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2013.
Uongozi na Utawala wa Mkoa umekuwa ukibadilika mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya Kitaifa. Tangu Mkoa uanzishwe hadi sasa Mkoa umeongozwa na jumla ya Wakuu wa Mikoa 18 kwa vipindi tofauti.
Orodha ya Wakuu wa Mikoa waliofanya kazi Mkoani Singida tangu uanzishwe ni kama ifuatavyo:
1. Bw. Dantes Ngua 1963 – 1964
2. Bw. Peter Kisumo 1964 – 1965
3. Bw. Rajabu Semvua 1965 – 1969
4. Bw. Kapilima Kapilima 1969 – 1971
5. Bw. Kingunge N. Mwiru 1971 – 1972
6. Bw. Moses Nnauye 1972 – 1975
7. Bw. Charles Kileo 1975 – 1977
8. Brigedia Silas Mayunga 1977 – 1978
9. Bw. Abdallah Nungu 1978 – 1981
10. Capt. Peter N. Kafanabo 1981 – 1986
11. Prof. John B. Machunda 1986 – 1987
12. Maj. Gen. Mwita C. Marwa 1987 – 1990
13. Bw. Gallus N. Abedi 1990 – 1993
14. Bw. Abubakary Y. Mgumia 1993 – 1997
15. Col. Anatoli N. A. Tarimo 1997 – 2002
16. Bibi Halima Y. Kasungu 2002 – 2006
17. Dr. Parseko V. Kone 2006 – 2016
18. Mhandisi Mathew J. Mtigumwe Machi - Disemba 2016
19. Dkt Rehema Nchimbi Disemba 2016 - Mei 2021.
20. Dkt Binilith Saatano Mahenge Mei 2021 hadi sasa
Kwa upande wa ngazi ya Mtendaji Mkuu wa Serikali katika Mkoa, Serikali ya Mkoa imekuwa inaongozwa na Wakurugenzi wa Maendeleo wa Mkoa tangu mwaka 1972 na baadaye mwaka 1997 chini ya Sheria Na. 19 ya Tawala za Mikoa – (Regional Administration Act Na. 19) Makatibu Tawala wa Mikoa (Regional Adiministrative Secretaries – RAS) waliteuliwa kuongoza Sekretarieti za Mikoa ikiwa ni njia ya kuimarisha uwajibikaji na utoaji huduma bora kwa wananchi.
Wakurugenzi wa Maendeleo walioongoza Mkoa tangu 1972 ni kama ifuatavyo:-
1. Bw. M. Jabiri Kigoda 1963 – 1964
2. Bw. C. M. Joachim 1972 – 1974
3. Bw. C. L. Kombo 1974 – 1975
4. Bw. Crispin Duncan Mbapila 1976 – 1977
5. Bw. I. Abubakar 1978 - 1983
6. Bw. L. M. Rimisho 1984 – 1985
7. Bw. A. S. Kaduri 1985 – 1988
8. Bw. A. A. K. Mwasajone 1988 - 1989
9. Bw. T. N. Machume 1989 – 1991
10. Bw. Fredrick Nyelwa Kisenge 1991 – 1994
11. Bw. Alfred Francis Fuko 1994 – 1995
12. Bw. Emanuel Petro Mazalla 1995 – 1997
Makatibu Tawala wa Mkoa waliouongoza Mkoa tangu mwaka 1997 ni kama ifuatavyo:-
1. Bw. Martin Odilo Mgongolwa 1997 – 2004
2. Bw. Zawadiel Mchome 2004 – 2006
3. Bibi Dyness G. Senyagwa 2006 – 2007
4. Bw. Hussein A. Kattanga 2007 – 2009
5. Bw. Godfrey S. Ngaleya 2009 – 2010
6. Bw. Liana A. Hassan 2010 – 2015
7. Bw. Festo L. Kang’ombe 2015- 2016
8. Dkt. Angelina M. Lutambi May 2016 - Juni 2021.
9. Bi. Dorothy Aidan Mwaluko Juni 2021 hadi sasa
ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZA WAKUU WA MIKOA WALIOWAHI KUFANYA KAZI MKOANI SINGIDA;
Mhe. Dantes Ngua - Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1963-1964 (wa kwanza kushoto)
Mhe. Peter Kisumo – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1964-1965 (aliyevaa kiraia)
Mhe. Rajabu Semvua – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1965 – 1969
Mhe. Kapilima Kapilima – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1969 – 1971
Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1971 – 1972.
Mhe. Moses Mnauye – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1972 – 1975 (aliyevaa miwani)
Mhe. Charles Kileo – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1975 – 1977
Mhe. Sailus Mayunga – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1977 – 1978
Mhe. Abdallah Nungu – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1978 – 1981
Mhe. Peter Kafanabo – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1981 – 1986
Mhe. John Machunda – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1986 – 1987
Mhe. Meja Jenerali Mwita Marwa – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1987 – 1990 (aliyesimama mbele)
Mhe. Galusi A. Abedi – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1990 – 1993
Mhe. Abubakari Mgumia – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1993 – 1997
Mhe. Kanali Mstaafu Anatol Tarimo – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 1997 – 2002
Mhe. Halima Kasungu – Mkuu wa Mkoa kwa mwaka 2002 – 2006
Mhe. Dk. Parseko V. Kone – Mkuu wa Mkoa kuanzia mwaka 2016.
Mhe. Mhandisi Mathew John Mtigumwe kuanzia Machi mwaka 2016 mpaka Disemba 2016.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida. Haki Zote Zimehifadhiwa.