Maendeleo ya Elimu katika Mkoa wa Singida yamekuwa yakiimarika mwaka hadi mwaka. Maendeleo haya ni pamoja na kuboreshwa kwa miundombinu shuleni; kuanzishwa kwa Shule za Binafsi na za Serikali na pamoja na kuongezeka kwa asilimia za ufaulu katika Mitihani ya Taifa.
Seksheni hii ina lengo la kusaidia au kuwezesha utoaji huduma za uendelezaji wa Elimu ikijumuisha usimamizi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na inayotolewa katika njia isiyo rasmi; na mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Huduma za Elimu
•Kuratibu uongozi wa shule za awali, Msingi, Sekondari, elimu ya watu wazima na Elimu rasmi
•Kuratibu ajira na usambazaji wa walimu wa shule za awali, msingi na sekondari katika Mkoa
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Elimu na mafunzo ya ufundi ndani ya Mkoa na kutoa Ushauri kadiri inavyohitajika.
•Kusimamia mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu katika Mkoa.
•Kuratibu ukusanyaji, tathimini, uunganishaji/uandaaji, kutafsiri na kutoa taarifa/takwimu za elimu na mafunzo ya ufundi katika Mkoa
•Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa taarifa za ukaguzi
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya utekelezaji wa sera ya utamaduni na michezo
•Kuratibu shughuli zinazohusiana na michezo katika Mkoa na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Mkoani.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida. Haki Zote Zimehifadhiwa.