Saturday 12th, October 2024
@SINGIDA
Maafisa Elimu wote na Wakuu wa shule mkoani Singidawametakiwa kutumia mbinu mbalimbali kusimamia taaluma ili kuhakikishaufaulu unaongezeka katika shule za msingi.
Maelekezo hayo yametolewa leo naKatibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga wakati alipokutana na Wakuu washule na Maafisa elimu Mkoa, Maafisa elimu Wilaya, Maafisa elimu kata Mkutanouliofanyika Katika ukumbi wa mikutano ulipo katika shule ya Sekondari St.Bernard.
Akiwa katika kikao hicho RASamewataka Maafisa elimu kuwa watatuzi wa changamoto za Walimu ikiwa nipamoja na kuzitembelea shule na kuja na mikakati ya kuboresha elimu kwakuhakikisha kila mwalimu anatimiza majukumu yake na kufanya kazi kwa ushindani.
Ameagiza wakuu wa shule kuwa nakawaida ya kufanya tathimini ya kila wiki kwa walimu na masomo wanayoyafundisha ili kubaini mapungufu na namna ya kutatua ambapo amesemaitasaidia kuwapima kutokana na matokeo.
Dkt. Mganga amesema ni wakati sasawalimu hao pamoja na watendaji wengine wakiwemo maafisa elimu kutoka maofisikwenda kwenye shule ambazo zinachangamoto ili kuinua hali ya elimu kwa kufanyatathmini ya wanafunzi ambao wanashindwa kuwa na matokeo mazuri.
“Twendeni tukafanye kazi, tuacheubosi, twendeni tukafanye tathmini tujue mwanafunzi gani anachangamoto ipi ilituweze kuzikabili changamoto ambazo zinaturudisha nyuma kiwango cha elimukwenye mkoa wetu”. Alisema Dkt. Mganga
“Kiongozi unaweka mikakati ilikuweza kupata matokeo usisikilize Rumors tumia jitihada zako upate matokeo iliuweke Legacy”. Aliongeza Katibu Tawala huyo.
Dkt. Mganga aliongeza kwa kusemakuwa viongozi wa Mkoa wa Singida wanapaswa kufanya kazi kwa kujituma ili wawezekuweka alama hivyo akasisitiza walimu wakuu kujituma na kujitoa zaidi kwenyekutoa elimu kwa wanafunzi.
Afisa Elimu Msingi Wilaya yaBahi, Boniface Willson ambaye alikuja kuwajengea uwezo walimu wa mkoa waSingida alisema kuwa mwaka 2017 Halmashauri ya Bahi ilikuwa na shule ambazozilikuwa hazifanyi vizuri kwenye elimu msingi hadi ikapewa bendera nyeusilakini baada ya kufanya tathimini kwa sasa imekuwa ikifanya vizuri.
Willson alisema kujituma kwawalimu wakuu kwenye Halmashauri hiyo ndiko kumeweza kubadilisha kutoka ufauluwa chini na sasa imekuwa moja ya Halmashauri inayofanya vizuri ndani ki mkoahadi kitaifa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.