WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo amempongeza hadharani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bw. Justice Kijazi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya eneo hilo kwa gharama ndogo sana ikilinganishwa na uhalisia.
Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake kupitia mfumo wa ‘force account’, wameweza kutumia kiasi cha sh. 420 milioni pekee kujenga ukumbi wa mikutano wa kisasa na wenye viwango, na 200 kujenga jengo kubwa la ofisi, huku akisisitiza kwa kuzitaka halmashauri ambazo bado hazijaanza ujenzi wa majengo ya ofisi na kumbi za kisasa za mikutano kuja kujifunza Ikungi.
Waziri Jaffo akiwa kwenye ziara ya kawaida mkoani Singida, na kupata fursa ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya, na miradi mingine ya halamshauri akitokea Jijini Mwanza, alisema katika uongozi wake amepita kwenye halmashauri nyingi lakini hajawahi kukutana na jengo la ukumbi mzuri na wa kisasa kama huo wa halmahauri ya Ikungi.
“Mkurugenzi kilichonifurahisha ni namna mlivyozingatia thamani ya pesa(value for money) na ubora, nilisema nataka ofisi ya TAMISEMI ifanye mabadiliko na mapinduzi ya kiutendaji, tulikotoka huko nyuma hatukuwa na sifa nzuri, lakini leo hii kila mahali ukitazama ikiwemo hapa ikungi huwezi kuamini,” alisema
Alizitaka halmashauri za Kondoa na Iramba kwa kuanzia kuja kujifunza kupitia wenzao hao wa Ikungi, ambao idadi ya majengo yao yote yamegharimu sh 1.5 bilioni pekee “nataka wengine wakitaka kujenga ofisi waje kujifunza hapa, iwe duplicate kwa wengine kuja kucopy na kupaste,” alisema Jaffo
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo alisema kiasi hicho cha pesa sh 1.5 bilioni kilitolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa halmashauri hiyo kwenye eneo la utawala bora.
Alisema kati ya pesa hizo sh 1.3 milioni zimetumika kujenga ofisi, nyumba ya DC, na Hospitali ya wilaya, huku Serikali ikiwa tayari imewatengea fedha nyingine zaidi ya sh. milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa vituo vya afya vya Sepuka, Ihanji na Iyumbu.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Bw. Justice Kijazi, alisema tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo mwaka 2013, watumishi wa eneo hilo wamekuwa wakipanga na kukodi majengo ya watu binafsi kwa mikutano mbalimbali, ikiwemo kutumia hadi nyumba za wageni kwa shughuli za ofisi.
Kijazi alisisitiza kuwa jengo la ukumbi huo mpya na wa kisasa mbali ya kutumika kwa shughuli mbalimbali za mikutano ya kikazi, lakini pia litatumika kama kitega uchumi cha kuingizia halmashauri hiyo mapato, huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Juma Ali Mwangi, akimuomba Waziri Jaffo kusaidia mchakato wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya kwa ustawi wa afya ya wakazi wa eneo hilo.
Hata hivyo, pamoja na kufurahishwa na Ikungi lakini hakufurahishwa na utendaji na usimamizi wa miradi ya vituo 2 vya afya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Iramba (Ndago na Kinampanda), ambavyo kwa mda mrefu ujenzi wake umekuwa ni wa kusuasua.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akizungumza na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali muda mfupi mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa ajili ya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi iliyopo katika Manispaa ya Singida na Ikungi mkoani Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo (watatu kutoka kulia) muda mfupi mara baada ya kuwasili katika kituo cha afya cha Sokoine katika halmashauri ya Manispaa ya Singida ambapo amelidhishwa na huduma, usimamizi na utendaji kazi unaoendelea kutolewa kwa wagonjwa katika kituo cha afya cha Sokoine Manispaa ya Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo (kushoto) akizungumza na Mtaalamu wa Maabara Bi. happyness Nyaruke katika kituo cha afya Sokoine
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akitia saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ikungi kabla ya kuanza ziara ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo mkoani Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo (wapili kutoka kushoto) akipokea ufafanuzi zaidi juu ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi Hagai Mziray wa kampuni ya Mzinga Holding (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri hiyo mkoani Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo (katikati) akipokea maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Bw. Justice Kijazi (kushoto) juu ya ujenzi wa ofisi na ukumbi wa halmashauri hiyo.
MUONEKANO WA BAADHI YA MAJENGO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe. Juma Ali Mwangi akizungumza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Bw. Justice Kijazi akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Bw. Edward Mpogolo akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
KIKAO KIKIENDELEA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama na Serikali pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.